Baada ya kuwepo kwa tetesi za wawili hao kutoka kimapenzi na zaidi kuonekana picha wako pamoja kwenye moja ya eneo za kula bata wakati wa usiku, ENewz ilimtafuta rapa Jay Moe avunje mzizi huo wa fitna kama ni kweli anaanguka kwa Shilole lakini alikanusha nakusema ndio mara ya kwanza yeye kusikia habari hizo.
"Ndio kwanza nasikia mambo hayo, sijui mamneno hayo yametoka wapi, ni mambo ya muziki tu na uvumi wa stori tofauti, kama picha mimi ni msanii na kama wasanii picha ni kawaida tu ila hakuna kinachoendelea kati yangu na Shilole"
Jay Moe anatajwa kuwa karibu na Shilole kutokana na urafiki wake na Billnas.
Post a Comment