Aliyekuwa mgombea ubunge Jimbo la Kahama Mjini katika Uchaguzi Mkuu mwaka jana kwa tiketi ya Chadema, James Lembeli amesema hana mpango wa kurudi CCM.
Lembeli alisema licha ya chama hicho kupata Mwenyekiti mpya kimejaa wanafiki, hivyo siyo kazi rahisi kurejea katika chama chake cha zamani.
Akizungumza kwa simu kutoka kijijini kwake, Bulungwa katika Halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama jana, Lembeli alisema anashangazwa na kitendo cha makada wa CCM kumpigia simu wakiwa Dodoma wakidai mbona hakurejea ndani ya chama hicho.
Post a Comment