Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako amesema wanafunzi wote wanaosoma vyuo vikuu wasio na sifa wataondolewa bila kujali wapo mwaka wa ngapi na hata waliopo kazini wataondolewa kwa kuwa hao ndio wanatumia njia za mkato kwenda kupata kazi japokuwa hawana sifa.
Waziri amevitaka vyuo vikuu kuchukua wanafunzi walio bora ili kuweka sifa ya ubora wa vyuo vyao
Na kuhusu vyuo vilivyochukua fedha ambazo hazikustahili vitalazimika kurudisha fedha hizo na kisha kuchukuliwa sheria kwa waliohusika, amesema bado wanaendelea kugundua idadi kubwa ya wanafunzi mfu walioombewa fedha tangia waanze zoezi hilo na sasa wamefikia vyuo vitatu tu.
1 comments:
no comment
ReplyPost a Comment