Loading...

Polisi Yasema Trafiki Aliyeuwawa Kijitonyama sio Yule Mwenye Mbwembwe

Usiku wa July 22 2016 ilisambaa taarifa ya kupigwa risasi Askari wa kikosi cha usalama barabarani wa kituo cha Polisi Oysterbay Kinondoni Dar es salaam ambapo alipigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa ni wahalifu wakati akiwa kazini katika eneo la Sayansi Kijitonyama.

Kutokana na mauaji hayo kutokea kwenye eneo la Sayansi taarifa zilizosambaa mitandaoni zilianza kumuhusisha na tukio hilo Askari mwingine wa barabarani aitwae Ashraf ambaye wengi ndio wamezoea kumuona kwenye eneo hilo kwa mbwembwe zake za kukimbiza foleni.

Baada ya kusambaa kwa taarifa kwamba aliyeuwawa ni yule Trafiki mchangamfu kwenye taa za barabarani, kamishna wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Simon Sirro kujua ukweli.

Kamanda Sirro amesema aliyeuwawa ni mwingine aitwae Mensah na sio yule Trafiki mwenye mbwembwe (Ashraf Shaban) ambaye amejipatia umaarufu hivi karibuni kutokana na uchangamfu wake barabarani na spidi yake ya kuondoa foleni akiwa kazini.

Post a Comment

CodeNirvana
Newer Posts Older Posts
© Copyright BAKI NASI | Designed By BAKI NASI
Back To Top