Loading...
Home
»
COMEDY
»
MATUKIO
»
NEWS
»
HIZI ZILIKUPITA: Sentensi Tano NZITO za Yusuph Makamba Kwenye Mkutano Mkuu wa CCM
Leo July 23 2016 Mjini Dodoma unafanyika mkutano mkuu maalum wa CCM ambao ajenda yake kubwa ni ya kumchagua Rais Dk. John Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa chama cha Mapinduzi ‘CCM’. Baada ya hotuba ya Mwenyekiti wa chama hicho Jakaya Kikwete, katibu mkuu mstaafu Yusuph Makamba alipata nafasi ya kuzungumza na kusema haya……
'Askofu Gwajima alisema uongo kwamba Jakaya Kikwete hakutaka kumpisha Magufuli kuwa mwenyekiti' - Yusufu Makamba #MkutanoMkuuCCM
'Chama kinatoka mikononi mwa kada anayekataa ufisadi kiasi cha kumtosa rafiki yake Lowassa'- Yusuph Makamba #MkutanoMkuuCCM
'Chama kinakwenda mikononi mwa muasisi wa Mahakama ya mafisadi'-Yusuph Makamba #MkutanoMkuuCCM
'Wapinzani nataka mjue JK alikuwa anawabatiza kwa maji huyu ajaye atawabatiza kwa moto'-Yusuph Makamba #MkutanoMkuuCCM
'Rais Magufuli hakukataa ushauri alikataa vimemo kikiwemo cha kwangu, kuna mtu nilikuwa nampigia debe awe DC'-Yusuph Makamba #MkutanoMkuuCCM
Post a Comment